Communiversity

Afrikan Language Institute => KiSwahili Language Resources => Topic started by: Dukuzumurenyi PhD on Feb 13, 2016, 03:04 AM

Title: Mapisi ya kiswahili [ahmed sheikh nabhany]-gctid175417
Post by: Dukuzumurenyi PhD on Feb 13, 2016, 03:04 AM
Chanzo

Kiswahili ni lugha miongoni mwa lugha za Kibantu. Tamko hili la Kiswahili linatokana nalugha ya KiaAmwu nalo ni sahil maana yake Pwani au Mwambao Je, jina hili ambalo limetokanana lugha ya KiaAmwu, wao wenyewe Wa-Bantu walikuwa hawana jina la kujiita katika lughayao? Jawabu laa! Lilikuwepo, nalo ni Wangozi na lugha yao Kingozi Wangozi ina maana yakabila, kama makabila mengine katika ulimwengu.

Waandishi wengi wameandika juu yaWaswahili na wanamapisi ya mapokezi walioeleza kwamba kabila kuitwa Wangozi ni kuwamatumizi makubwa yao walikitumia ngozi, viriba vya maji, viriba vya kuvugutia moto kwawahunzi au wafua chuma, kitapa cha kuchotea maji, viatu, kanda, nyuo za panga na visu hatakanda za kupimia ardhi na kadhalika Wangozi si kwamba walitumia ngozi kuwa walikuwa niwawindaji au ni wafugaji na ndipo wakaitwa Wangozi, kwa wanamapisi waandishi hawakubaliwanamapisi mapokezi, na ni jambo la kusikitisha kuwa wana fikra hiyo, wakizingatia hilamapokezi uandishi walipata maelezo kwa wanamapisi mapokezi ndipo wakaweza kuandikamapisi na mambo mengineo, wanamapisi maandishi vanataka ushabidi ili waamini kwamaandishi, kuwa asili ya Waswahili ni W angozi, ushahidi uliopo ni kwamba lugha ya Kiswahilicha zamani kinajulikana kwa jina la Kingozi na washairi wengi walijua jina hili kuitwa tungo zazamani zimeandikwa kwa Kingozi.
                            Attached files  2_04_nabhany.pdf (https://www.abibitumi.com/wp-content/uploads/ppMigration/175417=9199-2_04_nabhany.pdf) (753.8 KB)