Communiversity

Afrikan Language Institute => KiSwahili Language Resources => Topic started by: KaNisa on Aug 13, 2008, 05:42 PM

Title: Semi za Kiswahili (swahili sayings)-gctid30426
Post by: KaNisa on Aug 13, 2008, 05:42 PM
Semi za Kiswahili (swahili sayings)
 Semi ni vifungu vya maneno yenye maana fiche - Words that have hidden meanings.
 
 Hi ni baadhi ya semi chache nime kunited snakesnya
 
 NB: KEY
 
 m.y. - Maana yake (its meaning)
 
 mat. - Matumizi (how to use)

1. Ambukia patupu
 m.y. - Kosa kabisa
 mat. - Aliyekuwa akitafuta kitu kwa bidii sana na akakikosa anaweza
 kujisikitikia kwa kusema: Nimejitahidi juu chini lakini nimeambukia
 patupu.
 
 2. Ajabu ya shingo kukataa kulia mto
 m.y. - kataa kitu ulicho na haja kubwa nacho
 mat. - Usemi huu huambiwa mtu aliye na haja na kitu lakini ajifanya hana
 haja nacho. Basi aweza kuambiwa: Vipi bwana? Hiyo ndio ajabu ya shingo kukataa kulalia mto
 
 3. Amejifunga kwa ulimi wake
 m.y. - Amesema maneno ambayo yanathibitisha hatia yake.
 mat. - Mshtakiwa aropokaropokaye kortini anaweza kuonywa na wakili
 wake kwa kuambiwa: Utajifunga kwa ulimi wako iwapo
 hutazungumza kwa hadhari
 
 4. Amekwenda mrisi
 m.y. - Hajafanikiwa katika aliyotaka
 mat. - Usemi huu waweza kuutimia hivi: Alitaka kuwa mbunge lakini mpaka sasa ameenda mrisi..

5. Ametumbukia kisimani
 m.y. - Ameingia katika shida ambazo ni vigumu kujitoa